Huyu ni mwanangu mpendwa ninayependezwa naye...
Katika Biblia kuna amri iliyotoka kwa
Mungu..."MISIKIENI YEYE!" Mungu alinena hayo
kuhusu mwanawe Yesu. Kama hujui
yatakayotokea kwako baada ya kufa. Basi soma
kikaratasi hiki.(1) Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simuhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu ila niokoe ulimwengu. Yeye anikataye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amuhukumuye; neno hilo nililoli-nena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Yohana 12:47-48MSIKIENI YEYE! Ukimkataa Yesu, utahukumiwa na neno lake siku moja.
(2) "Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu, kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu." Yohana 8:24 "Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu." Warumi 3:23MSIKIENI YEYE! Usipomwamini Yesu utakufa na dhambi zako. (3) "Mimi ndimi njia na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." Yohana 14:6MSIKIENI YEYE! Yesu alisema huwezi kufika mbinguni ila ya yeye
hakuna njia nyingine.(4) Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha hukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.MSIKIENI YEYE! Kama hujaamini Bwana Yesu, wewe
umeshahukumiwa tayari katika ziwa la moto.(5) "Kwa maana mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilicho-potea." Matayo 18:11MSIKIENI YEYE! Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote,
kwa maana hapana jina njingine chini ya mbingu
walilopewa Wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo." Matendo 4:12(6) "Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu." Warumi 10:3MSIKIENI YEYE! Unahitaji haki ya Mungu - Bila hiyo utaenda kuzimu
sasa hivi. Pokea haki yake Mungu."Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu." I Yohana 1:9Sasa hivi, tafadhali muombe Yesu Kristo aje moyoni
mwako, akuokoe na akusamehe makosa yako."Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika watu, utaokoka." Warumi 10:9 (7) "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe." Matayo 24:35MSIKIENI YEYE! "Maneno yalionenwa na Yesu hudumu ya kweli leo, kesho, na hata milele. Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu." Waebrania 9:27Je, umefahamu ya kwamba mstari huu wa Biblia
umedhihi-rishwa kuwa kweli. Ni ukweli mtupu ya
kuwa siku moja utakufa...na ni kweli utahukumiwa na
maneno yalio-nenwa na Yesu!q Ni chaguo langu kumkataa Yesu.
"Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu nami nita-mkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni." Matayo 10:33MSIKIENI YEYE! "Asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia." Yohana 3:36bq Nimekubali kumkiri Yesu awe Mwokozi wangu.
"Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu." Yohana 10:28 "Yeye aliye naye mwana, anao huo uzima; asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima." Yohana 5:12Tafadhali tutumie karatasihii utujulishe ya kwamba
baada ya kulisoma, umekata kauli ya kumpokea
Yesu awe Mwokozi wako.Jina __________________________________
Anwani _______________________________
Mji _____________________ Umri _________
[ Christian Helps Ministry (USA) ] [ Christian Home Bible Course ]